Breaking

Post Top Ad

MBAPPE NI ZAIDI YA MESSI, RONALDO


KOCHA mkongwe Jose Mourinho anaamini umri wa Kylian Mbappe ukilinganisha na uwezo alionao, unamfanya awe na thamani zaidi ya masupastaa, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Fowadi huyu wa Paris Saint Germain, 20, tayari ameshabeba Kombe la Dunia, Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) mara mbili, ameshafunga jumla ya mabao 55 kwenye ligi na ameshakamata nafasi ya nne kwenye Ballon d’Or, yote hayo kabla hajafikisha miaka 21.

Mourinho ambaye ni kocha wa zamani wa Manchester United, anaamini umri wa dogo huyo ndiyo unaomfanya awe na thamani kwenye soko la usajili zaidi ya nahodha wa Barcelona, Messi, 31, na straika wa Juventus, Ronaldo, 34.

“Kwa mchezaji kama Mbappe, huhitaji kusema atakuwa katika kiwango gani miaka mitano au kumi ijayo. “Ukichukua umri wake, ukalinganisha na wa Cristiano, Messi, wote wakiwa na zaidi ya miaka 30, Neymar ana 2, unapokwenda kwenye soko la usajili, ni mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi,” alisema Mourinho

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US