Breaking

Post Top Ad

KWA WAPENDA SOKA HII SI YA KUKOSA!!!!!!!!

Image result for SIMBA SHAGWE

Uongozi wa Simba umetangaza kiingilio cha Sh 3,000 hadi Sh 100,000 kwa mashabiki wake wanaotaka kushudia mechi ya mwisho ya Kundi D ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya AS Vita.
PAKUA APPLICATION YETU   CLICK TO DOWNLOAD
Tofauti na mchezo uliopita dhidi ya Al Ahly viingilio vilitangazwa na bilione Mohamed Dewji, leo aliyechukua jukumu hilo ni Afisa Habari, Haji Manara.
Manara ametangaza bei ya chini ya tiketi za kuingia uwanjani ni Sh 3000, mzunguko wakati VIP B, itakuwa Sh 10,000 na VIP A, itakuwa Sh 20,000.

PAKUA APPLICATION YETU   CLICK TO DOWNLOAD
Mbali ya kuwepo na tiketi hizo ambazo zimezoeleka kutakuwa na tiketi za Platinum zitakuwa zikiuzwa kwa Sh 100,000 kwa watu maalumu.

PAKUA APPLICATION YETU   CLICK TO DOWNLOAD
Wawakilishi hao wa Tanzania wataingia katika mchezo wa siku ya Jumamosi dhidi ya AS Vita kwa malengo mawili kwanza kulipa kisasi cha kufungwa mabao 5-0 jijini Kinshasa, pili kuhakikisha wanashinda na kusonga mbele
Katika mechi hiyo Simba wenye pointi sita kama watamfunga AS Vita wenye pointi saba watakuwa wamefuzu hatua ya robo faibali wakisibiri mechi ya Al Ahly na JS Saoura ili kufahamu imemaliza katika nafasi ya kwanza au pili.

PAKUA APPLICATION YETU   CLICK TO DOWNLOAD
Mchezo huo muhimu kati ya Simba dhidi ya AS Vita utachezwa Uwanja wa Taifa saa 1:00 usiku

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US