Breaking

Post Top Ad

BADO HAAMINI MACHO YAKEKOCHA wa timu ya AS Vita Florent Ibenge amesema kuwa ameshangazwa namna alivyofungwa na kikosi cha Simba Uwanja wa Taifa kwani alijiandaa kushinda kwenye mchezo huo uliowapoteza mazima kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ibenge ambaye ni kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Congo, kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Congo alishinda kwa mabao 5-0 hali iliyomfanya aamini angetumia nguvu hiyo kutinga hatua ya robo fainali.

Ibenge amesema kuwa kwenye mchezo huo alianza vizuri na wachezaji wake walijitimu ila baada ya kufunga bao la kwanza walijisahau wakadhani wapo nyumbani hali iliyowapa nafasi Simba kusawazisha.

"Tulianza kwa mipango mikali ya kutafuta bao la mapema na hilo tulifanikiwa, wachezaji wangu walijisahau wakadhani tumeshinda hali iliyowapa nafasi wapinzani wetu kusawazisha.

"Kwenye chumba cha kubadilishia nguo niliwapa mbinu mpya ila zote ziligoma na nikashanga mpira unaisha tumefungwa mabao 2-1, lakini yote ni matokeo hivyo nawapongeza Simba maana tuliwafunga nyumbani kwetu na wao wametufunga," alisema Ibenge.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US