Breaking

Post Top Ad

Arsenal, Chelsea na kibarua kizito Europa

Image result for europa league today
Usiku wa leo zitachezwa mechi za kwanza za hatua ya 16 bora ambapo timu za Chelsea na Arsenal zinategemewa kufuzu kwenda hatua inayofata. Chelsea watakuwa nyumbani dhidi ya Dynamo Kyiv, timu ambayo imeshiriki kwa muda mrefu sana katika mashindano makubwa ya Ulaya, wameshiriki mfululizo tangu msimu wa 1989/90.
Arsenal watakuwa ugenini kwa Rennes kucheza mchezo wa kwanza – Naye kiungo wa timu hiyo Grani Xhaka alisema wamejipanga kufanya vizuri. “Ukishinda Europa League unaenda moja kwa moja kwenye Champions League. Lakini bado naamini Premier League ni nafasi yetu nzuri kufikia Ligi ya mabingwa.
” Sevilla (vs Slavia Prague) na Valencia (vs Krasnodar) wataanza safari ya kuitafuta robo fainali wakiwa nyumbani huku Villarreal watasafiri takriban kilomita 4000 kuwafata Zenit St Petersburg. Napoli wanacheza dhidi ya Red Bull Salzburg huku Inter wakianzia ugenini kwa Frankfurt. Mchezo wa Chelsea dhidi ya Dynamo Kyiv utachezwa saa 5:00 Usiku na ule Arsenal vs Stade de Rennais FC ni saa 2:55 Usiku.
Zote mbili zitaonyeshwa Mubashara kupitia chaneli ya ST World Football HD Michezo mingine ya Europa kama Inter vs Frankfurt na Napoli vs RB Salzburg itaonyeshwa kupitia chaneli

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US