Breaking

Post Top Ad

Apple kutoa simu tatu mwaka 2019

Kampuni ya Apple Inc imepanga kuzindua simu tatu za iPhone kwa mwaka huu zikiwa na vipengele kadhaa vya kuvutia ikiwemo kuwa na kamera tatu, imeripoti jarida la Wall Street.

Apple watatoa simu hizo mpya zikiwa na muonekano sawa na iPhone XR lakini zikiwa na vipengele kadhaa vipya na bora zaidi hii ni kutokana na kudorora kwa mauzo ya simu za iPhone XR nchini Uchina ambako ndio soko kubwa la simu za mkononi duniani.
Aidha, Apple yenye makao makuu yake Cupertino, California, imeamua kuendelea kutumia vioo vya teknolojia ya Liquid-Crystal Display (LCD) kwa wakati huu, lakini ikiweka wazi kwa mwaka 2020 kuanza kutumia vioo vya OLED baada ya iPhone XR kushindwa kufanya vyema ikiwa na kioo cha LCD.
Apple wanatazamiwa kuhamia kwenye teknolojia ya USB Type C kwenye simu zao zijazo.

Wiki iliyopita Apple ilitoa taarifa ya kushuka kwa hisa zake kwa asilimia 10, kitu ambacho hakijatokea kwa miaka 12 iliyopita.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US