Breaking

Post Top Ad

TAMKO LA MASOUD DJUMA BAADA YA KUPIGWA CHINI SIMBA HILI HAPA


Baada ya kuoneshwa mlango wa kutoka nje rasmi, Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma, amesema kuondoka ndani ya wekundu wa Msimbazi si mwisho wa kuendelea na maisha mengine.

Djuma ambaye alitua Simba mnamo mwezi Oktoba 2017, aliteka vichwa vya habari baada ya kuripotiwa kukosa maelewano mazuri na Makocha wakuu tofauti ndani ya timu hiyo.

Mrundi huyo ameeleza kuwa kuondoka Simba ni mwanzo wa yeye kuendelea na maisha mengine ya soka na akisema kuwa Simba si sehemu pekee atakayokaa milele.

Kocha huyo aliingia kwenye migogoro na Mfaransa, Pierre Lechantre ambaye aliondoka na kumpa mikoba Mbelgiji Patrick Aussems ambaye anaendelea kukinoa kikosi cha Simba mpaka sasa.

Migogoro na kutokuelewana baina ya Djuma na wakuu wake yaliendelea kushika kasi, ikiwemo kuelezwa kusababisha chuki binafsi baina ya wachezaji na mkuu wake, jambo ambalo Aussems hakulifurahia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US