Breaking

Post Top Ad

MOURINHO AWAGEUZIA GIA WACHEZAJI UNITED


Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anasema baadhi ya wachezaji wanajali zaidi, baada ya klabu hiyo kukosa kushinda katika mechi tatu za karibuni zaidi walizocheza.

Katika mechi mbili za majuzi zaidi walizocheza United ligini, walitoka sare na Wolves lakini wakashindwa na West Ham.

Kwa sasa wameshuka hadi nafasi ya 10 kwenye Jedwali la Ligi ya Premia.

Aidha, walitupwa nje ya klabu ya Derby kutoka michuano ya Kombe la Carabao.

Kwa mujibu wa BBC, alipoulizwa kama ana wasiwasi kuhusu kazi yake iwapo klabu hiyo itaendelea kuandikisha matokeo mabaya, Mourinho alijibu: "La hasha."

Mourinho alikuwa akizungumza kabla ya United kukutana na Valencia lao katika mechi ya hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

"Kila mchezaji ni tofauti, wachezaji hawafananai," alisema.

"Naviona vitendo tofauti, lakini kile unachoona si kile kilichomo ndani.

"Huwa naona kwamba nawakera watu, baadhi ya watu ambao huwa hawaonekani ni kama wameshindwa kwenye mechi.

"Naona hivi hivi, lakini katika vikao viwili vya mazoezi tulivyokuwa navyo (tangu Jumamosi) kila kitu kilikuwa kawaida, hamu ya kutaka kutia bidii na kucheza."

Mourinho aliongeza: "Kile ninachoweza kukifanya kuboresha mambo huwa nakitenda, na nitaboresha mambo ambayo yananitegemea mimi na kazi yangu."No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US