Breaking

Post Top Ad

THIS IS SIMBA BROTHER!! MASHABIKI WAFURIKA UWANJA WA NANGWANDA SIJAONA MUDA HUU
Wakati pambano la mechi ya Ligi Kuu huko Mtwara kati ya Ndanda FC dhidi ya Simba likusubiriwa kwa hamu, unaambiwa mwitikio wa mashabiki umekuwa mkubwa.

Foleni kubwa ya mashabiki wa timu hizo mbili huku wageni ambao ni Simba wakionekana kuleta hamasa kubwa katika dimba la Nangwanda Sijaona wameanza kumiminika ndani ya Uwanja huo.

Mashabiki hao wamejitokeza kwa wingi katika uwanja huo ili kuweza kushuhuia mechi hiyo ambayo ina motisha ya aina yake leo Jumamosi.

Simna inakutana na Ndanda ikiwa na rekodi ya kutopoteza alama tatu tangu walima korosho hao wapande daraja kushiriki Ligi Kuu Bara mwaka 2014.

Mechi hiyo itaanza majira ya saa 10 kamili jioni ambapo itakuwa mbashara kupitia kituo cha Azam TV.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US