Breaking

Post Top Ad

MWINGINE MMOJA AJIENGUA YANGA


Wakati kikosi cha Yanga kikiwa kinashuka Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza mchezo wa kirafiki na African Lyon, kuna uwezekano mkubwa wa Nahodha wake, Kelvin Yondani kukosena.

Ukiachana na wachezaji Juma Abdul, Juma Mahadhi na Abdallah Shaibu walio majeruhi, Yondani naye ni anaweza akaukosa mchezo huo.

Yondani alishindwa kujumuika na kikosi cha Stars kilichoelekea Uganda kwa ajili ya kucheza mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2019 dhidi ya Taifa hilo.

Kwa mujibu wa Daktari wa kikosi cha Stars, Richard Yomba, alisema beki huyo aliumia mguu hivyo ikabidi wambakize Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.

Yondani alikabidhiwa rasmi mikoba ya Unahodha Mkuu ndani ya Yanga baada ya aliyekuwa akivaa kitambaa hicho, Nadir Haroub Cannavaro kustaafu soka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US