Breaking

Post Top Ad

YANGA YAPATA VIKOSI VITATU MOROGORO


Mashabiki wa soka bado hawajakiamini kikosi cha Yanga, lakini Mwinyi Zahera amewaambia kwamba kambi ya Morogoro imempa vikosi vitatu ambavyo vinaundwa na mchanganyiko wa wachezaji chipukizi na wakongwe.

Kikosi cha kwanza kati ya hivyo ni kile kinachoundwa na kipa, Klaus Kindoki kutoka DR Congo, Juma Abdul, Gadiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondani, Feisal Salum ‘Fai Toto’ Deus Kaseke, Papy Tshishimbi, Mrisho Ngassa, Rafael Daud pamoja na Heritier Makambo.

“Ukiachana na kikosi hicho kikosi cha pili kinaweza kuundwa na kipa, Beno Kakolanya, Paul Godfrey, Haji Mwinyi, Pato Ngonyani, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ Juma Makapu, Juma Mahadhi, Thaban Kamusoko, Emmanuel Martin, Amisi Tambwe na Ibrahim Ajibu.

“Kikosi cha tatu nilichokipata ni kile kinachoundwa na wachezaji wengi ambao ni chipukizi wakiongozwa kipa, Ramadhan Kabwili, Jafar Mohammed, Mohammed Issa ‘Banka’, Pius Buswita, Maka Edward, Said Mussa, Matheo Anthony, Yusuph Muhilu na kuna wachezaji wengine kama watatu hivi wa kutoka kikosi cha vijana ambao nao ni wazuri,” alisema Zahera.

 “Kutokana na ubora wa vikosi ndiyo maana najiamini kuwa nitafanya vizuri ligi kuu kwani ikitokea mchezaji mmoja ameumia yupo wa kuziba nafasi yake tena kwa ustadi mkubwa ukizingatia baada ya kuondoka Hassan Kessy wengi walijua kuwa nafasi ya beki wa kulia amebakia Juma Abdul peke yake.

“Lakini ukweli ni kwamba, pengo hilo nimefanikiwa kuliziba na sasa nafasi hiyo inawachezaji zaidi ya watano wanaoweza kuicheza vizuri, wawili wanatoka kikosi cha vijana na wengine ni Ninja, Pato lakini pia Mahadhi anaweza kuicheza vizuri nafasi hiyo,” alisema Zahera.

Mfumo ambao Zahera amekuwa akitumia mazoezini ni kushambuliana kwa kasi huku pia wachezaji wote wakipigwa marufuku kupiga pasi za nyuma pasipo sababu yoyote ya msingi, pasi ambazo walitakiwa kupiga ni za kwenda mbele tu, jambo ambalo walionekana kulifanya kwa ustadi mkubwa

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US