Breaking

Post Top Ad

YANGA WAGOMA KUMSAKA MBADALA WA MANJI KUELEKEA UCHAGUZI UJAOBaada ya uongozi wa Yanga kuanza mchakato wa uchaguzi kwa ajili ya kuwapata viongozi walioachia ngazi, imeelezwa kuwa Kamati ya Uchaguzi imeamua kuibakisha nafasi ya Mwenyekiti wa klabu.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya hapo awali kuelezwa kuwa Yanga waliamua kuanza mchakato huo wakiwa na lengo la kumpata pia mbadala wa Mwenyekiti huyo lakini wameamua kugeuza gia angani na badala yake haitotumika kwenye uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ndani ya klabu hiyo, Bakili Makele, amesema bado wanamtambua Yusuph Manji kama Mwenyekiti wao hivyo kutakuwa na nafasi ya kumsaka Makamu na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji pekee.

Licha ya Manji kutuma barua ya kuomba kujizulu nafasi yake akiomba apumzike kutokana na kubanwa na mambo kadhaa, klabu hiyo ilipinga barua hiyo kupitia mkutano mkuu uliofanyika jijini Dar es Salaam Juni 10 2018.

Makele amesema Yanga bado inajua kuwa Mwenyekiti wake ni Manji hivyo nafasi yake ikiendelea kuwepo kama kawaida.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US