Breaking

Post Top Ad

WATATU SIMBA KUIKOSA TANZANIA PRISONS LEO


Kikosi cha Simba kianshuka dimbani leo majira ya saa moja jioni kuanza rasmi pazia la Ligi Kuu Bara kwa kucheza na Tanzania Prisons.

Kuelekea mchezo huo Simba itawakosa wachezaji wake watatu ambao ni Mlinda mlango Deogratius Munishi 'Dida', Kiungo Clatous Chama na Mganda Emmanuel Okwi.

Dida na Chama watakosekana katika mchezo huo kutokana na kukosa Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ambazo mpaka sasa bado hazijawasili.

Aidha, Mganda, Emmanuel Okwi naye atakosekana baada ya kuumia katika mchezo wa Ngao ya Hisani uliopigwa jijini Mwanza Agosti 18 ndani ya dimba la CCM Kirumba.

Simba itaanza pazia la michuano hiyo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam majira ya saa moja za usiku ili kuwapa nafasi watazamaji kufurahia sikukuu ya Eid uzuri zaidi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US