Breaking

Post Top Ad

SIMBA WAWASILI MWANZA TAYARI KUKIPIGA NA MTIBWAKikosi cha Simba kimeondoka jijini Arusha asubuhi ya leo kuelekea Mwanza tayari kwa mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Sugar.

Simba watacheza na mabingwa hao wa Kombe la Shirikisho Tanzania kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kesho majira ya saa 10 kamili jioni.

Wakati Simba wakikwea pipa na sasa wakiwa tayari wameshawasili Mwanza, taarifa zinaeleza kuna uwezekano mkubwa wa Nahodha wake, John Bocco kucheza mchezo huo.

Bocco hajacheza mechi yoyote tangu kumalizika kwa ligi msimu wa 2018/19 kutokana na kupatwa na majeraha lakini kuna uwezekano akacheza dhidi ya Mtibwa hiyo kesho.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US