Breaking

Post Top Ad

SIMBA WATOA TAMKO LAO BAADA YA MANJI KUREJEA YANGA


Simba wamesisitiza kwamba hawahofii kitendo cha Yu­suf Manji kurejea Yanga kama mwenyekiti na kwamba hawezi kuathiri kwa vyovyote mipangilio yao.

Manji alitangaza Jumapili iliyopita kure­jea Yanga na mzuka wake uliwapa wache­zaji nguvu ya kuwapiga USM Algiers mabao 2-1 kwenye mechi ya Shirikisho.

Tathmini inaonyesha kwamba uwepo wa Manji Yanga kutaibua upinzani mkubwa miongoni mwa timu hizo mbili kongwe kwenye kutokana na Simba kuwa na kiburi cha muwekezaji, Mohammed Dewji ‘MO’.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tully alisema kuwa, wao hawamhofii Manji na badala yake wanapam­bana kuona timu yao inafanya vyema msimu huu.

“Sisi hatuna upinzani na Manji bali tuna upin­zani na Yanga na hatujali uwepo wake na badala yake tutapambana kuhakikisha tunafanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu.”

Simba ndiyo klabu iliyosajili wachezaji ghali zaidi msimu huu tofauti na klabu zingine zinazoshiriki ligi hiyo ambayo inaanza leo bila mdhamini mkuu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US