Breaking

Post Top Ad

Ricardo ni kivuli cha Xavi na Iniesta

Katika maisha yake pale klabu aliisaidia Barcelona kutwa ubingwa wa UEFA Youth League: 2017–18 akiwa amefunga mabao matatu na kutengeneza mengine matatu.
Mechi yake ya kirafiki dhidi ya Ac Milan alifanya makubwa sana licha ya kupewa dakika 45 tu. Kwa dakika hizo kuna watu walisema kuwa kwa namna anavyogusa mpira ni kama Andrés Iniesta na ana upeo mkubwa wa kufikiri kama legendi mkubwa wa Barcelona Xavi.
Kocha mkuu wa Ernesto Valverde alimwagia sifa nyingi sana bwana mdogo yule kwa uwezo wake mkubwa alipoonesha.
Kucheza pembeni ya Lionel Messi kwake ni ndoto kubwa. Ni heshima ya kipekee akiwa na miaka 18 kufanikiwa kumpa pasi Messi. Inampa motisha.
Messi wakati anaanza soka lake alimkuta Dinho. Kila mara alioofunga Dinho alimbeba Messi mgongoni. 
Image result for messi ronaldinho
Huu ni mtihani mkubwa sana Ernesto Valverde katika kuwaamini vijana wa La Masia kama ilivyokuwa kwa Frank Rijkaard aloyemtoa Messi, Pep Guardiola akamtoa Sergio Busquets, Johan Cruyff akamtoa Guardiola na Louis Van Gaal akamtoa Xavi.yakati naamini kuwa ili ufanikiwe unahitaji daraja la kukuvusha. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US