Breaking

Post Top Ad

MOURINHO AFUNGUKA


Jose Mourinho amewaambia rafiki zake kwamba angeweza kujiuzulu kutoka klabu nyingine yoyote kufikia sasa ila si Manchester United. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 anaarifiwa kutafshika kwa anachokiona kuwa ni ukosefu wa kuungwa mkono na kaimu mwenyekiti Ed Woodward. (Mirror)

Licha ya kutafshika, Mourinho anasalia kuwa na uwajibikaji mkubwa katika klabu hiyo ya Old Trafford. (Manchester Evening News)

Aliyekuwa mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane ana hamu kuipata nafasi kuiongoza Manchester United iwapo tu Mourinho ataondoka. (Mail)

Bin amu wa mmiliki wa Manchester City Sheikh Mansour ameshindwa kuinunua Liverpool kwa thamani ya £ bilioni 2b. (Mail)

Danny Rose wa Tottenham analengwa na Paris St-Germain wanaotaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Ulaya. (Mirror)

Real Madrid bado inashughulika kumsajili mchezaji atakayeichukua nafasi ya Cristiano Ronaldo na inaamini ina nafasi ya kumpata mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, aliye na miaka 19. (Marca - kupitia Metro)

Klabu hiyo ya Uhispania sasa inahisi 'huenda haitowezekana' kumsajili mojawapo ya washambuliaji wakuu katika ligi ya England katika dirisha hili la uhamisho na sasa wanaelekeza azma yao kwa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Valencia Rodrigo, kando na Mbappe. (Independent)

Aliyekuwa mshambuliaji wa Liverpool Iago Aspas, 31, anahitajika na Real Madrid na huenda akaondoka Celta Vigo kwa mkataba wa thamani ya £ milioni 35. (Super Deporte - kupitia HITC)

Real Betis wamewasilisha rasmi ombi la kumsajili mchezaji chipukizi wa Manchester City mwenye umri wa miaka 21 Oleksandr Zinchenko kwam kataba wa mkopo kwa msimu mzima, kwa mtazamo wa kumpa mkataba wa kudumu. (Mundo Deportivo - kupitia Manchester Evening News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US