Breaking

Post Top Ad

MODRIC, COURTOIS, MANCHESTER, LEWANDOWSKI, MARTIAL: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYAReal Madrid wameweka tangazo la kiwango cha bei ya £670m kwa mchezaji wa miaka 32 wa kiungo cha kati wa timu ya Croatia -Luka Modric, aliyetajwa kama mchezaji bora wa Kombe la Dunia la 2018, kuizuwia Inter Milan kujaribu kumchukua. (Mirror)

Belmadi apewa mikoba ya kuinoa Algeria
Manchester United imeafiki masharti binafsi ya mlinzi wa Barcelona Yerry Mina, mwenye umri wa miaka 23, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia akisubiri klabu ziukubali mkataba . (Metro, via Mundo Deportivo)

Winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 25, amewaambia wachezaji katika timu yake kwamba yuko tayari kuondoka Crystal Palace na anaweza kuwasilisha maombi ya kuhamia Chelsea. (Mirror)

Barcelona imekubali masharti binafsi ya mchezaji wa Bayern Munich Arturo Vidal, huku mchezaji huyo wa kiungo cha kati wa Chile mwenye umri wa miaka 31- akitarajiwa kuigarimu timu hiyo ya Championi ya Uhispania £27m. (Guardian)

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amejipanga kwa mazungumzo na mlinda lango Thibaut Courtois, huku Real Madrid wakiwa tayari kusaini mkataba na Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 26 . (Diario AS, via Star)


Chelsea wanamtaka mchezaji wa Real Madrid Mateo Kovacic baada ya mchezaji wa kiungo cha kati kuripotiwa kukataa kuhamia Manchester United kwasababu ya mtindo wa mchezo wa Jose Mourinho' . (Express, via Calciomercato)
Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumtoa mshambuliaji wake kutoka Ufaransa Anthony Martial, mwenye umri wa miaka 22, kwa Bayern Munich kama sehemu ya mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, mwenye umri wa miaka 29. (Mirror)

RNGM blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US