Breaking

Post Top Ad

MMOJA KUONGEZA NGUVU YANGA IKIFANYA MAAJABU MBELE YA WAARABU TAIFA LEO
Kikosi cha Yanga kinashuka dimbani leo kukipiga dhidi ya USM Alger katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika kipute hicho kitakachoanza majira ya saa 1 za usiku, Yanga itamtumia straika wake ambaye amekuwa tegemeo baada ya kung'ara Morogoro, Heritier Makambo kutokana na kupata kibali kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Straika huyo aliyesajiliwa kutoka FC Lupopo ya Congo, alishindwa kukipiga dhidi ya Gor Mahia kwenye mchezo wa mkondo wa pili ikiwa ni wiki mbili zilizopita na kupoteza kwa mabao 3-2.

Ujio wa Makambo unaipa nguvu Yanga ya kufanya vema kwenye safu ya ushambuliaji ndani ya kikosi ambayo mpaka sasa imefunga mabao mawili pekee katika mechi nne za kundi D na ikiwa na alama moja pekee mkiani.

Yanga wamerejea jijini Dar es Salaam jana wakitokea Morogoro ambako waliweka kambi ya wiki mbili na kufikia kwenye hoteli ya Protea, ilioyopo maeneo ya Posta kupata mlo wa usiku kabla ya kuwavaa USM Alger leo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US