Breaking

Post Top Ad

MASHABIKI MAN U WAMVAA MTENDAJI WA KLABU


Mashabiki wa Manchester United wamelipia bango kubwa litakalokuwa linapepea hewani wakati wa mchezo kati ya timu yao dhidi ya Burnley likitaka Mtendaji wa Man United, Ed Woodward, aondoke kwenye klabu hiyo.

Tukio hilo litatokea Jumamosi ya wiki ijayo kwenye Dimba la Turf Moor, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu England baina ya timu hizo.

Tukio hilo limekuja baada ya kocha Jose Mourinho, kulalamika mara kwa mara kuwa bosi huyo alishindwa kutoa fedha za kutosha za usajili.

Inaaminika kuwa bango hilo litakuwa limeandikwa ‘Ed Out – LUHG’, ikiwa ni ishara ya kwanza kuwa bosi huyo hatakiwi na mashabiki. LUHG ikiwakilisha Love United, Hate Glazers, yaani Ipende United, Wachukie Glazers (wamiliki wa klabu)

Mashabiki wa timu hii walikuwa wa kwanza kutumia mbinu ya mabango kumuondoa aliyekuwa kocha wao, David Moyes.

Lakini pia Arsenal waliwahi kutumia njia hiyo pia wakati wa vuguvugu la kuondolewa kwa kocha, Arsene Wenger.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US