Breaking

Post Top Ad

Mambo MAWILI katika kolabo ya Harmonize na Professor JayMsanii wa muziki Bongo kutokea WCB, Harmonize ameweka wazi kuwa wimbo unakuja kati yake na Professor Jay.

Harmonize ameeleza ilikuwa ni ndoto yake ya miaka mingi kufanya kazi na Professor Jay. Wakati tukisubiria kolabo hiyo itoke, kuna kuna mambo mawili ya kukumbuka.


Mosi; Harmonize atakuwa msanii wa pili kutokea WCB kufanya wimbo na Professor Jay baada ya Diamond Platnumz ambaye alishirikishwa na rapper huyo katika wimbo uitwao Kipi Sijasikia ambao ulitoka mwaka 2014 . 

Wimbo huo ulikuwa wenye mafanikio makubwa ambapo mwaka 2015 ulishinda tuzo kupitia Kilimanjaro Music Awards (KTMA) kama wimbo bora wa Hip Hop. 


Pili; Professor Jay anakuwa msanii mwingine wa Hip Hop Bongo kufanya kazi na Harmonize baada ya Young Killer kumshirikisha muimbaji huyo katika wimbo wake uitwao Unaionaje. Yes!, ni Young Killer ambaye mwaka 2014 alishinda tuzo ya KTMA kama msanii Bora Anayechipukia.


RNGM blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US