Breaking

Post Top Ad

Kuna kipindi Diamond alikufaa moyo kuhusu Harmonize - Babu Tale


Meneja kutokea WCB, Babu Tale amesema kuwa kuna kipindi Diamond Platnumz alikata tamaa kuhusu Harmonize kutokana na mwenendo wa muziki wake kwa kipindi hicho.

Meneja huyo akipiga stori na Wasafi TV amesema kuwa hata hivyo baadaye kama uongozi waliona msanii huyo hakuwa na makosa bali ni maneno kutoka nje ndiyo yaliyopelekea hayo yote.

"Kuna kipindi Diamond alikufaa moyo kuhusu Harmonize na ikibidi tumsimamishwe kwa makosa ambayo si ya kwake kwa makosa ambayo ni maneno tunaletwe kutoka nje," amesema.  

"Baadaye tukasema tusisikilize maneno, hawa watu hawawezi kutusaidia, huyu ni biashara yetu sisi acha tukomae nayo , kesho na kesho kutwa tutakaa sawa, Mwenyenzi Mungu amesaidia Harmonize anapata mkate wake wa kila siku," ameongeza Babu Tale.

Harmonize ndiye msanii wa kwanza kusainiwa na label ya WCB na wimbo wake wa kwanza kutoa ni Iyola. Baada yake ndipo wakafuata wasanii wengine kama Rayvanny, Rich Mavoko, Queen Darleen, Lava Lava na Mbosso.

RNGM blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US