Breaking

Post Top Ad

HII NDIYO SABABU YA CHAMA KUWAKOSA MTIBWA NGAO YA JAMII MWANZA LEO
Kiungo mpya wa klabu ya Simba, Clatous Chama, ataukosa mchezo wa leo ambao timu hiyo inacheza dhidi ya Mtibwa Sugar jijini Mwanza.

Simba inakipiga na Mtibwa kwenye mechi ya Ngao ya Hisani itakayoanza majira ya saa 10 kamili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Kwa taarifa ambazo zipo zmezithibitisha kutoka kwa uongozi wa klabu hiyo ni kuwa Chama hatokuwepo Uwanjani kutokana na Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kuchelewa kufika nchini.

Kiungo huyo ambaye alionesha ufundi mwingi kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana Agosti 8, alisajiliwa kutoka Dynamo FC ianyoshiriki Ligi Kuu Zambia.

Katika orodha ya wachezaji wa Simba watakocheza mchezo huo, jina la Chama limekosekana sababu ya ITC yake kuchelewa hivyo kuna uwezekano akaanza kukipiga pindi ligi itakapoanza.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US