Breaking

Post Top Ad

BAADA YA MANJI KUREJEA YANGA


Uongozi wa Yanga umesema kuwa kurejea kwa Yusuph Manji klabuni hapo kutaamsha fuaraha amani na umoja baada ya kuwa kwenye kipindi cha mpito.

Yanga imekuwa ikipitia wakati mgumu kwa takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu Mwanachama huyo atangaze kujiengua nafasi yake ya Uenyekiti wa klabu.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kitendo cha Manji kuhudhuria mchezo wa Kombe la Shirikisho jana wakati timu yao ikicheza dhidi ya USM Alger kutoka Algeria kutaamsha ari ya zamani.

Ten amesema kurejea kwa Manji kutarejesha hata mshikamano ndani ya klabu ikiwemo wachezaji kujituma na hii ni kutokana na kuendelea kuichezea timu huku wengi wakiwa hawajalipwa mishahara kwa muda mrefu.

Hata hivyo Manji hakutamka kama amerejea rasmi kwenye nafasi yake japo dalili zinaonesha uwezekano mkubwa wa kurudi upo.

Katika mchezo wa jana, Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kufanikisha kupata ushindi wa kwanza huku ikifikisha alama 4 kwenye kundi D.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US