Breaking

Post Top Ad

BAADA YA KUKOSA MDHAMINI MANARA ASEMA LIGI ITAKUWA YA TIMU MBILIOfisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema kuna dalili kubwa ya msimu ujao ligi kwa na washindani wakubwa wawili ambao ni Simba na Azam FC.

Hatua hiyo imekuja kufuatia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukosa wadhamini wakuu wa ligi mpaka sasa baada ya Kampuni ya Mawasiliano Vodacom kumaliza mkataba wake.

Manara ameeleza Azam na Simba wanaweza kuleta ushindani pekee kutokana na kuwa vizuri kiuchumu tofauti na klabu zingine ambazo zinapitia changamoto kifedha.

"Kwa namna hali ilivyo kwa timu nyingi kuna uwezekano mkubwa ligi inaweza ikawa na ushindani wa klabu mbili pekee ambazo ni Simba na Azam, hivi vingine vina hali ngumu itakuwa changamoto kwao".

Aidha, Ofisa huyo amewashauri TFF waendelee kupambana kumsaka mdhamini ili aweze kuja kuwa suluhisho la matatizo kwa timu zingine huku akisema kama inawezekana wamtafute ili awasaidie kumtafuta.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US