Breaking

Post Top Ad

WhatsApp kupambana na taarifa za uongo

taarifa za uongo
Hatua hii imekuja baada ya watu kadhaa kupigwa na wengine kuuawa kwa sababu ya taarifa za uongo kusambazwa kupitia njia ya ujumbe wa WhatsApp.

Tatizo la usambazaji wa taarifa zisizo za kweli mitandaoni limeendelea kuisumbua WhatsApp kiasi cha kuanza kuweka udhibiti maalum wa kuendelea kusambazwa kwa habari za uongo.

Watumiaji wa WhatsApp karibuni wataanza kuwekewa udhibiti idadi ya kutuma ujumbe wanaowasambazia watu wengine pamoja na makundi mbalimbali ya WhatsApp.

Taarifa iliyotolewa na WhatsApp wenyewe inasema watumiaji wataweza kusambaza jumbe 20 tu huku nchi kama India wakiruhusiwa kusambaza takribani jumbe 5 Nchi za India, Myanmar na Sri Lanka zimeripotiwa mara kadhaa kukumbwa na mauaji, utekaji uliosababishwa na jumbe za uongo za WhatsApp.

Mfumo wa ujumbe wa WhatsApp wa ‘end to end encryption‘ umewafanya WhatsApp wenyewe kutojua kinachotumwa hivyo kushindwa kuzuia ujumbe wa uongo unaosambazwa kupitia programu tumishi ya WhatsApp.

WhatsApp imeahidi kuendelea kudhibiti taarifa za uongo, huku India yenye watumiaji milioni 200 wa WhatsApp ikiongoza kwa usambazaji wa habari za uongo ikifuatiwa na Brazil.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US