Breaking

Post Top Ad

Utani wa Idris Sultan kwa Alikiba, Diamond baada ya Jokate kuteuliwa na JPM


Bila shaka unakumbuka jana July 28, 2018 Rais Dk. John Pombe Magufuli alifanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya mbalimbali, miongoni mwa walioteuliwa ni Mwanamitindo na Mjasiriamali, Jokate Mwegelo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

Sasa basi, Mchekeshaji Idris Sultan kwenye moja ya post zake Instagram ameweka picha ya Alikiba na Diamond na kuandika; 'Asiyesikia la mkuu haioni Kisarawe #JopoLaKisarawe'.

Utakumbuka kuwa Diamond na Alikiba walishakuwa na mahusiano na mrembo huyo kwa vipindi tofauti.

Katika hatua nyingine katika post ya Jokate katika mtandao huo baada ya kukaa kimya kwa zaidi ya miezi mitatu, Idris ame-comment hivi; I don't care what you just said i'm just happy it's you... "Best role model kwa my future daughter".

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US