Breaking

Post Top Ad

Shilole awabania mashabiki MwanzaMsanii wa Bongo Flava ambaye haishiwi vioja kila siku "Shilole" amesema hawezi kucheza kwenye Tamasha hilo huku amewageuzia mashabiki nyuma kwani ameolewa na ana mheshimu mumewe.

Shilole ameyasema hayo leo katika Tamasha la Komaa jijini Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba lililoandaliwa na EFM, ambapo alipopanda jukwaani mashabiki walimuomba ageuke nyuma ndio wanapenda hiyo staili ya uchezaji wake tofauti na akiwa anawaangalia kwani wanaboeka.


"Mie nina mume jamani, nyie tatizo hampendi kuniona mbele mnataka nicheze nimegeuka nyuma ndio mana nina madensa wangu wanageuka staili zote za kucheza na kama mnavyowaona wanajua kunengua sana," amesema.

Msanii huyo alizidi kuwakazia mashabiki wake kuwaonyesha uchezaji wake wa zamani na kuubeza ni wa fujo, kwani amekuwa wa kitofauti huku amemilikiwa  na hapendi kumuumiza ampendaye japo wanaume wengi wana wivu ndio na kwamba analijua hilo na halimsumbui na siyo kwa huyo mume wake pekee hata kwa mwanaume mwingine.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US