Breaking

Post Top Ad

Mitazamo Ya DJ Zerro Na @MwanaFA / Sifa Za DJ Mkali JukwaaniMoja kati ya marapa wakali nchini Mwana FA amesema moja kati ya vitu vigumu ambavyo hawezi kufanya ni kuimba juu ya wimbo wake mwenyewe, Au kuimba kwenye sound mbovu. 

 “Moja kati ya vitu vigumu ambavyo siwezi kufanya ni kuimba kwenye sound mbovu au kuimba juu ya wimbo wangu, unajua mimi huwa nategemea beat na chorus tu, Siwezi kuimba kwenye sound mbovu, namwambia DJ azime muziki nipige Acapella, imeshanitokea mara kadhaa nashindwa kuvumilia hata nafokea madj mbaya zaidi Nikikutana na DJ mwenye kichaa jukwaani”.
 Mwana FA ameyasema hayo wiki iliyopita kwenye XXL ya Clouds FM Radio.


Akijibu swali la mtangazaji BDOZEN aliyetaka kujua sifa za DJ mzuri  wakati wa Perfomance, DJ maarufu nchini DJ Zerro amesema Sifa ya dj mzuri ni kuisoma Cloud na sio kumfuta msanii anavyotaka,

“Dj Mzuri ni Yule anayeweza kuusoma mzuka wa mashabiki wanaomuangalia msanii jukwaani wala sio DJ kumsikiliza sana msanii.

“Wasanii wengi wanapenda kuperform na mimi kwasababu wanajua najua kucheza na mizuka yao,
DJ mzuri ni Yule  anayeweza kuisoma ‘Cloud’ na kujua nini kinawashawishi na sio kusikiliza maombi ya msanii anayeperfom muda huo.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US