Breaking

Post Top Ad

Miaka kumi ya App Store kwenye biashara
Changamoto, kupata faida/hasara kwenye biashara ni jambo la ambalo linafahamika na kwa namba inawezekana kuonekana ni ndogo lakini kwa yale waliyoyapitia katika kipindi cha miaka kumi sio kitu kidogo.

Mwezi Julai 2008 ndio soko la programu tumishi lililopo chini ya Apple lilianzishwa na lilikuwa na programu tumishi 500 tuu. Mwazilishi mwenza wa Apple, marehemu Steve Jobs alitabiri Apple Store itakuwa na mafanikio na ndio kitu kinachoonekana kwa sasa.
Katika kipindi cha muongo mmoja App Store imeweza kuwa soko la programu tumishi takribani milioni 2 mpaka hivi sasa.

Katika kipindi cha mwezi ilipoanzishwa iliweza kuwa na programu tumishi 11,500 na kuweza kuwalipa waliozitengeneza takribani $21 milioni.


Mafanikio ya App Store yamechagizwa na nini?

Wakati fulani kwenye mahojiano Steve Jobs aliulizwa kufanikiwa kwa App Store kumetokana na nini? Akaweka wazi sababu/vipengele vikuu viwili tu; mahtaji na mabadiliko ya teknolojia.
Kwanini mahitaji? Katika mwezi mmoja tu takribani milioni 60 waliweza kupakuwa programu tumishi kutoka kwenye App Store. Hivi leo idadi ya wanaopakuwa programu mbalimbali kutoka kwenye soko la programu tumishi lililo chini ya Apple imeongezeka sana.
Mabadiliko ya teknolojia. Hiki ni kitu ambacho hakopingiki, kutokana na teknolojia kubadilika imekuwa ni chanzo cha mapato kwa wengi na kwa upande wa wanaounda programu tumishi mpaka mwaka 2018 wameweka kupata jumla ya $100bn kutoka $21 milioni miaka 10 iliyopita
Marehemu Steve Jobs aliona kuwa miechezo (magemu) sio kitu cha kupuuzia hivyo aliwezaalweza kukaribisha magemu kama Nintendo na Sony handhelds ambapo magemu mengine yalikuwa yanapatika bure na mengine ni ya kulipia mpaka hivi leo.


App Store inaendelea kuwa na watu wengi wanaopita kwenye soko hilo kila siku kutokana na mahitaji ya kile ambacho kinaona kinawafaa kwenye simu zao. Miaka inaenda na haionekani dalili la soko hilo la programu tumishi kutetereka


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US