Breaking

Post Top Ad

Ijue simu mpya kutoka Motorola ya Moto Z3 Play
Sifa zinazofanya Moto Z3 Play ivutie.

Muundo wa Moto Z3 Play hautamshangaza yeyote yule kwani ni uleule wa toleo la nyuma yake. Na hii imefanywa kusudi ili kutoleta mkanganyiko kwa watumiaji na pia kupata muonekano wenye kufahamika zaidi kwa simu za Moto Z.
Tofauti kubwa ya toleo la Z3 Play ni kwamba sehemu kubwa ya mbele ya simu imemezwa na kioo kama zilivyo simu rununu za kisasa. Pia ina wembamba mzuri na kuifanya simu kuvutia na kushikika kwa urahisi zaidi.
Kingine cha kuvutia ni ukubwa wa kutosha wa sauti; ina sauti (speaker) ambayo hutahitaji kuweka sikioni kama mpenzi wa kusikiliza muziki na sauti za hotuba au simulizi mbalimbali kwenye simu yako, hili litakufurahisha zaidi.
Simu hii ina ulinzi wa kutumia alama ya kidole ambapo mwenye simu atakuwa hana wasiwasi wowote wa simu yake kudukuliwa na mtu mwingine; kidole chaki, simu yako.
Kwa upande wa kioo cha Z3 Play ni starehe sana kwa mtumiaji wake. Kidole hakitapata tabu sana. Ni kiasi cha mguso kidogo tu na kile ulichokusudia kinafunguka. Aina ya kioo kilichotumika ni cha teknolojia ya Super AMOLED chenye ukubwa wa inchi 6.01.

Simu yenye kioo cha aina hii humfanya mtumiaji wake kufurahia rangi zenye ubora wa hali ya juu sana kuanzia mwangaza/giza lake kuwa katika muonekano unaomfanya mtumiaji kupendelea kuangalia kwenye simu yake bila ya kuumiza macho.

Kamera mbili za nyuma za Moto Z3 Play
Kwenye suala la Prosesa Z3 Play imewezeshwa na prosesa yenye ufanisi mkubwa ya Qualcomm Snapdragon 636 pamoja na kuwa na RAM yenye ukubwa wa 4GB au 6GB na uhifadhi wa ndani wa ukubwa wa 64GB au 128GB. Ukubwa wa RAM (6GB) na memori ya ndani (128GB) utapatikana kwa soko la Brazil tu kwa sasa.
Kwa upande wa betri ipo vizuri kwa kuwa na betri lenye 3,000mAh ambapo litamuhakikishia mtumiaji wake kutokuwa na wasiwasi wa kuishiwa chaji kirahisi na kwa haraka. Ni mwendo wa kuperuzi kurasa za intaneti na mambo mengine kadhaa bila khofu ya kuishiwa chaji.
 Unaweza kuweka MicroSD mpaka 2TB
Kwa upande programu kama kawaida Moto Z3 Play imeendelea kutumia mfumo endeshi kutoka Google wa Android 8.1 na uzuri wa simu za Moto ni kupata maboresho mapema kwa simu zake mara tu yanapokuwa tayari kuwafikia watumiaji wake. wa mambo ya picha picha, Moto Z3 Play haijawaacha nyuma kwani imewawekea kamera zenye uwezo mzuri wa kuchukua picha kwa mazingira yoyote na bado wakapata picha zenye kiwango bora.
Kamera za nyuma zipo mbili, moja inatoa picha za 12MP na nyingine 5MP na kwenye kamera ya mbele kwa watu wa Selfie ipo kamera yenye 8MP. Uzuri ukipiga picha za video kwenye simu ya Moto Z3 Play wakati unataka kuhifadhi kwenye simu yako unachaguo la namna gani unataka kuhifadhi. Moja ya chaguo unaweza kuhifadhi kwa mfumo wa GIF.

Simu hii imezinduliwa mwezi Juni na tayari imeanza kupatikana katika masoko mbalimabali duniani kwa kiasi cha dola 499.99 takribani sawa na shilingi za kitanzania 1,139,600.
No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US