Breaking

Post Top Ad

Bob Junior aeleza A-Z kuhusu kolabo yake na Diamond Platnumz
Msanii wa Bongo Fleva na Producer, Bob Junior amefunguka ilipoishia mipango ya yeye kufanya kolabo na Diamond Platnumz.

Bob Jonior akizungumza na Wasafi TV amesema kuwa licha ya mipango hiyo kuwepo bado nafasi ya kufanyika haijapatikana

"Mashabiki wake wakawa wananisumbua sana, nikamtafuta Diamomd tufanye huo wimbo mashabiki wananisumbua tufanya hii kazi, tunaongeza kabisa, tunapanga muda, sasa akawa bize," amesema Bob.

"Ndio siku nikasema sasa jamani eee, msione kama kuna kolabo bado hatujafanya na hata hii mipango tumekaa tumeongea naona yupo bize, so subirini itatokea itakuja," ameongeza.

Katika hatua nyingine Bob Junior amesema wimbo wa kwanza wa Diamond uitwao Kamwambie hakuchukua fedha yoyote bali fedha alikuja kuipata kutoka kwenye nyimbo nyingine za Diamond zilizofuatia.  


RNGM blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US