Breaking

Post Top Ad

Baada ya Jokate kuteuliwa na Rais Magufuli, Steve Nyerere acharuka
Hapo Jana July 28, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli alifanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya mbalimbali, miongoni mwa walioteuliwa ni Mwanamitindo na Mjasiriamali, Jokate Mwegelo.

Sasa basi, msanii wa Bongo Movie, Steve Nyerere amewataka wale wote wanaomtumia sms za pole kwa kuwa yeye hakuteuliwa waache mara moja. Kupitia mtandao wa Instagram ameandika.

"Mnao nitumia sms za pole naomba iwe mwisho sasa. Sipo kwa ajili ya cheo nipo kwa ajili ya Tanzania kwanza mengine hapana, msinilishe maneno," amesema Steve.

Hapo awali Steve Nyerere alimpongeza Jokate kwa kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kwa kumueleza kuwa anafahamu atasimama kidete kuhakikisha watu wa wilaya yake wanaendelea.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

CONTACT US